Nafasi ya Kazi Meneja Mradi Msaidizi – TRANS TANZ


Nafasi ya Kazi Meneja Mradi Msaidizi – TRANS TANZ

NAFASI YA KAZI YA MENEJA MRADI MSAIDIZI KATIKA SHIRIKA
LISILO LA KISERIKALI LA TRANS TANZ
TRANS TANZ ni shirika lisilo la kiserikali, linalojihusisha kusadia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuweza kupata huduma za kiafya kwa urahisi. Shirika hili linaendesha mradi unaotoa huduma ya kurahisisha wananchi kupata pesa ya usafiri wa kwenda kwenye kituo cha afya kuchukua dawa na kurudi majumbani kwa watu waishio na virusi vya UKIMWI.
Shirika la TRANS TANZ lilianza kufanya kazi wilayani Bagamoyo tangu mwaka 2009, mpaka leo bado shirika linaendesha mradi wa kusaidia waathirika wa virusi vya UKIMWI wilayani Bagamoyo. Shirika hili linatekeleza mradi huo katika Kituo cha Afya cha Miono na katika kituo cha afya cha Mbwewe. Lengo la mradi ni kuwasaidia wananchi walioathirika na virusi vya UKIMWI ambao wanatumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na wanaoishi mbali na vituo vya afya kupata nauli za kwenda kwenye kituo cha afya kuchukua dawa na kurudi majumbani mwao kila mwezi bila kuwa na changamoto ya kutokuwa na pesa ya nauli.
Shirika la TRANS TANZ linatafuta mtu mwenye sifa kufanya kazi ya Meneja Mradi Msaidizi. Mtu huyo awe na sifa au ujuzi kama ilivyoainishwa hapa chini:-


UJUZI UNAOHITAJIKA
 • Ujuzi wa kuandika na kuongea Kiingereza na Kiswahili
 • Uelewa wa changamoto wanazopata watu wenye maambukizi na
  wanaoishi na virusi vya UKIMWI
 • Ujuzi wa Teknohama, kwa mfano kutumia programu kama Excel, Word na Barua Pepe
 • Uwezo wa kusafiri mara moja kwa wiki kwenda kwenye vituo vya afya vifuatavyo, Miono, Mbwewe na Kwa Ruhombo
 • Uwezo wa kuwasiliana na watu kwenye jamii.
 • Uwezo wa kufanya Mahesabu
Also Read:
UJUZI UNAOTAFUTWA
 • Ufahamu kuhusu matibabu ya Virusi vya UKIMWI/UKIMWI katika mkoa wa Pwani.
 • Uelewa wa changamoto wanazopata watu wanaoishi na virusi vya
  UKIMWI.
 • Ujuzi wa Teknohama, kutumia programu kama Excel, Word, na Barua Pepe
 • Ujuzi wa kufanya kazi za kujitolea
 • Ujuzi wa kufanya kazi na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
 • Ujuzi wa kufanya kazi na wauguzi katika Sekta ya Afya katika Wilaya na na katika jamii kwa ujumla.
 • Ujuzi wa kukusanya taarifa na kuzipanga kwa usahihi.
KAZI NA MAJUKUMU.
 • Kuhudhuria katika vituo vya afya vyote ambavyo mradi wa Trans Tanz unatekelezwa mara moja kwa wiki.
 • Kukukusanya taarifa za kitabibu za Trans Tanz kwa kila wiki. (kwa mfano kwa mfumo wa sasa kuhudhuria siku moja katika kituo cha afya cha Mbwewe, siku mbili katika kituo cha afya cha Miono, na siku moja katika kituo cha afya cha Kwa Ruhombo kwa mpango wa baadae.
 • Kuwasiliana na waudumu wa afya kwa kila kituo na kuainisha changamoto na kuripoti kwa Meneja Mradi changamoto zinazojitokeza, mapendekezo na mafinkio ndani ya wiki hio.
 • Kulipa wahudumu wa afya, na kukusanya kumbukumbu za malipo hayo.
 • Kumsaidia Meneja wa Mradi kukusanya taarifa na kufanya mahesabu ya matumizi ya fedha.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
 1. Muombaji wa kazi ni lazima awe ni mkazi (anaishi) wa Bagamoyo.
 2. Barua ya Maombi na CV viandikwe kwa lugha ya Kiingereza pekee.
 3. Barua ya Maombi ni lazima iwe na anwani sahihi, namba za simu na barua pepe za muombaji, pamoja na anwani sahihi, namba za simu za wadhamini watatu
 4. Wakati wa kutuma Maombi usiambatanishe vyeti.
 5. Muombaji atagharimikia gharama zake mwenyewe atakapoitwa kwenda kwenye usaili.
 6. Maombi ya Kazi yatumwe kwenye anuani ya Barua Pepe ifuatayo:
  info@transtanz.org
 7. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe, Jumapili tarehe 31 Machi 2019
.
TAHADHALI: Usitoe Pesa kwa ili Upate Ajira