Tuesday, February 13, 2018

TANGAZO LA MAPITIO YA ‘KANUNI ZA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA ZA MWAKA 2016

Tags


Lengo la mapitio haya ni kuboresha kanuni hizi ili ziweze kuongeza  tija, ufanisi na weledi katika shughuli zifanywazo na Sekretarieti ya Ajira hususan uendeshaji wa michakato ya ajira kwa niaba ya Serikali.
Hivyo mdau wetu, mmoja mmoja, kikundi au Taasisi, unaombwa kutoa maoni yako ya kuboresha Kanuni zetu. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia barua pepe maoni@ajira.go.tz. Aidha unaweza kutumia anuani ifuatayo: Katibu, Sekretarieti  ya Ajira, S.L.P 63100 Dar  es Salaam au hata kuwasilisha maoni yako katika Ofisi zetu zilizopo ghorofa ya pili, Jengo la Maktaba (Barabara ya Bibi Titi Mohamed), Dar es Salaam. Muda wa mwisho wa kuwasilisha maoni ni tarehe 23 Februari 2018.
Kwa maelezo Zaidi wasiliana kwa namba zifuatazo: +255786284778 au +255754594655.
Nakala ya Kanuni hizi inapatikana katika tovuti hii ya www.ajira.go.tz katika eneo la “legislation”
Source: Tanzania Public Recruitment